Karibu Usharika Wa Mbezi Beach

WARUMI 1:16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

Ndugu msomaji wa tovuti hii, ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninakupongeza na kukushukuru kwa kufuatilia habari za ufalme wa Mungu katika tovuti hii. Usharika wa Mbezi Beach umejikita katika kuhubiri uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminie. Tunamuhubira Kristo ndani na nje ya nchi kwa njia mbalimbali ikiwemo , Ibada zetu, Semina za Neno la Mungu, Mikutano ya Injili, uimbaji, maombi na maombezi, na huduma za kijamii. Tunapokusanyika pamoja katika ibada zetu tunatamani kila anishiri akutane na Mungu pamoja na nguvu zake.

1 WAKORINTHO 2:4-5 , 4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, 5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Ibada zetu huwa zinaambatana na maombi na maombezi, tunamuona Bwana Yesu akiwaponya wengi, wasio na amani wanapata amani, waliofungwa na nguvu za giza wanafunguliwa na wengi wakizidi kuongezeka katika kumjua Mungu na kutakaswa kwa damu ya Yesu Kristo. Kila jumapili tuna ibada mbili moja inaanza saa 1:00 Asubuhi na nyingine saa 4:00 asubuhi ambazo huambatana na Ibada za watoto (Sunday School). Pia, tuna kipindi cha Fellowship kila Jumapili kuanzi a saa 10:00 jioni, mazingira ya kuabudia kiroho na kimwili ni muhimu sana kwetu ili kukutana na Mungu. Tuna ibada za katikati ya wiki kwa makundi mbalimbali kama inavoonekana kwenye taratibu vya ibada. Kila Jumatano kuanzia saa 11 tuna kipindi cha Bible study ambapo tunajifunza Biblia kwa kina. Kila siku ya Ijumaa kuanzi a saa 11 jioni ni saa ya ukombozi ; maombi na maombezi, wenye shida mbalimbali wanafunguliwa kwa Jina la Yesu Kristo. Pia tuna ibada za nyumba kwa nyumba ambazo hufanyika mara moja kila wiki kufuatana na mazingira ya fellowship husika. Ibada hizi zimekuwa baraka kubwa katika familia zetu kila tunapokutanika na kushirikiana katika mambo ya kiroho na kijamii. Tuna vikundi mbalimbali vya uimbaji pamoja na darasa la muziki kwa wanopenda kumtumikia mungu kupitia uimbaji na ala za muziki. Dira yetu kwa mwaka 2017 ni kuinua maisha ya kiroho ya washarika kama kiini cha mambo mengine yote, Mahubiri na Mafundisho ya Neno la Mungu,Maombi na mombezi, pamoja na huduma za udiakonia ni kipaumbele katika mwaka huu. Ninakukaribishi kushiriki katika huduma hizi. Unaweza kufuatia mafundisho mambalimbali na ibada zetu kupitia Utube katika account hii MbeziBeach Lutheran Church

Image Gallery

Popular LinksContact Us

K.K.K.T DAYOSIS YA MASHARIKI NA PWANI JIMBO LA KASKAZINI USHARIKA WA MBEZI BEACH

Address:Mbezi beach, Dar es salaam
Telephone: +255 22 2618117
P.O.Box:604331 DSM
E-mail: info@mbezibeachlutheran.org